Wadau mbalimbali wa soka wakiwemo wagombea wa uchaguzi katika nafasi mbalimbali za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wamekamatwa jijini Mwanza.
Baadhi ya waliokamatwa ni pamoja na Mtangazaji wa Clouds FM, Shaffih Dauda, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), Almas Kasongo.
Imeelezwa walikamatwa jana saa tatu usiku jijini humo wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ikiwa ni kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 12 mjini Dodoma.
Wengine waliokamatwa ni pamoja na Elias Mwanjale, Leonald Malongo, Effam Majinge, Osuri Kasuli, Richard Kayenzi, Lazack Juma na Kelvin Shevi.
Msemaji wa Takukuru jijini hapa, Ernest Makale amethibitishwa kukamatwa kwao na kusema wamehojiwa.
“Tumewahi na kuwaachia kwa dhamana, sasa uchunguzi unaendelea,” alisema.
Imeelezwa watuhumiwa walisema walifika jijini Mwanza kwa ajili ya uzinduzi wa michuano ya Ndondo Cup jijini humo.
Social Plugin