TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 18/07/2017
YAMETOKEA MATUKIO YAFUATAYO;
(1) AJALI YA TELA LA TREKTA KUPINDUKA , KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI. TAREHE 17.07.2017 SAA 06. 00 KATIKA KIJIJI CHA SOLWA,KATA YA
SOLWA,TARAFA YA NINDO,WILAYA YA SHINYANGA (V) MKOA WA SHINYANGA TELA YA TREKTA AINA YA MASSEY FERGUSON NO ZA USAJILI T 740 DJU LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA MTU AMBAYE HAJATAMBULIKA LILIPINDUKA NAKUSABABISHA KIFO CHA LUCAS S/OMETHUSELA,46YRS,MKULIMA,MSHASHI,MKAAZI WA SOLWA.PIA KUSABABISHA MAJERUHI KWA NDAMO S/O CHEREHANI,38YRS,MKULIMA,MSUKUMA,MPAGANI,MKAZI WA SHIRIMA.CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. UFUATILIAJI WA KUMTIA MBARONI DEREVA HUSIKA UNAENDELEA.
(2) AJALI YA MOTO KUUNGUZA BWENI NA KUTEKETEZA MALI. TAREHE 17.07.2017 MAJIRA YA SAA 0800 KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA BUNAMBIYU KIJIJI NA KATA YA BUNAMBIYU TARAFA YA MONDO WILAYA YA KISHAPU MKOA WA SHINYANGA WILFRED S/O JOHN, 28YRS MSUKUMA, MWALIMU WA SHULE YA SEKONDARI BUNAMBIYU ALIBAINI BWENI KUUNGUA MOTO NA KUTEKETEZA MALI ZA WANAFUNZI WA KIKE 26 WALIOKUWA WANALALA KATIKA BWENI HILO. THAMANI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO HAIJAFAHAMIKA HAKUNA MADHARA KWA BINADAMU. CHANZO CHA MOTO BADO KINACHUNGUZWA.
(3)AJALI YA NYUMBA KUUNGUA MOTO NA KUSABABISHA HASARA YA MALI. TAREHE 17.07.2017 SAA 16:00 HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MHUNZE YA JUU MJI MDOGO WA MHUNZE KATA,TARAFA, NA WILAYA YA KISHAPU MKOA WA SHINYANGA NYUMBA YA AMANI S/O ISSA, MIAKA 39,MSUKUMA, MKULIMA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA MHUNZE ILIUNGUA MOTO NA KUTEKETEZA MALI ZILIZOKUWEMO NDANI ZENYE THAMANI YA TSH:100,000,000/= HAKUNA MTU YEYOTE ALIYEDHURIKA CHANZO CHA TUKIO KINACHUNGUZWA.
(4) KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO KUWA YA WIZI.TAREHE 17/07/2017 SAA 15.00 MJINI KAHAMA MKOA WA SHINYANGA ASKARI WA KIKOSI CHA UPELELEZI WALIMKAMATA OBADIA S/O MUNYA, MIAKA 32, MUHA, MKULIMA NA MKAZI WA MHONGOLO AKIWA ANAUZA PIKIPIKI YENYE USAJILI NAMBA T559 BEZ, ENGINE NAMBA SL157FMI * 16906998* NA CHASSIS NAMBA * LBRSPJB57G9004812* AINA YA SUNLG HUKU AKIWA NA KADI YA KUGHUSHI AKIUZIA PIKIPIKI HIYO. MTUHUMIWA ANAHOJIWA KWA KINA NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO ZINAFANYWA.
(5)KUPATIKANA NA SILAHA AINA YA GOBORE (HOME MADE GUN) TAREHE 17/7/2017 SAA 14:00 KIJIJI CHA SHISHINULU,KATA YA NSALALA,TARAFA YA ITWANGI,WILAYA/MKOA SHINYANGA ASKARI POLISI WALIWAKAMATA WATU WAWILI (ME) WAKAZI WA KALIUA WAKIWA NA SILAHA/BUNDUKI TATU AINA YA GOBORE ZINAZODAIWA KUTUMIKA KATIKA VITENDO VYA UHALIFU KWENYE MKOA WETU NA MIKOA JIRANI NA WALIKUWA WAKIZIPELEKA KWA MGANGA WA KIENYEJI ILI KUFANYIWA MATAMBIKO. UPELELEZI WA KINA UNAENDELEA NA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
IMETOLEWA NA MULIRO J MULIRO (ACP ) RPC-SHY
Social Plugin