Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAIFA STARS YAIBAMIZA BAFANA BAFANA 1 - 0, YATINGA NUSU FAINALI




Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amethibithisha ubora wake mbele ya mwenzake wa Bafana Bafana, Stuart Baxter baada ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Elias Maguli dakika 17 ya mchezo huo.


Ushindi huo unaipa nafasi Stars kusonga mbele hatua ya nusu fainali katika mashindano hayo ya Cosafa.


Stars imewavua Bafana Bafana ubingwa wa Cosafa baada ya kuwafunga kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani.


Awali Kocha huyo wa Afrika Kusini alijinadi akisema anaamini kikosi hicho chenye vijana wengi kingeimaliza Stars, jambo ambalo limekuwa kinyume na matarajio yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com