Ikulu ya White House imesema kuwa Rais Donald Trump, anaunga mkono makubaliano yasiopendelea upande wowote yaliyoafikiwa katika bunge la Congress ya kuiwekea vikwazo Urusi.
Imesema kuwa Rais Donald Trump, anaunga makubaliano yasiopendelea upande wowote yaliyoafikiwa katika bunge la Congress ya kuiwekea vikwazo Urusi.
Afisa habari wa Ikulu ya White House Sarah Huckabee-Sanders anasisitiza kuwa, licha ya hatua hiyo awali white house ilipinga mswada wa uamuzi huo, japo kuwa kwa sasa inafurahia mswaada wa mwisho uliopitishwa.Putin amekana nchi yake kuhusika kuingilia uchaguzi huo
Bunge la Congress linataka Urusi iadhibiwe kwa madai ya kuingilia uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka jana nchini Marekani.
Bunge hilo linatarajiwa kupiga kura hapo kesho siku ya jumanne kupitisha muswada huo kuwa sheria inayoitaka ofisi ya Rais kutoingilia mwenendo wa hatua za kidplomasia dhidi ya Moscow.
Ikulu ya white house hata hivyo imekuwa na kauli zinazotofautiana mara baada ya msimamo wa bunge la Congress katika vikwazo vipya dhidi ya tuhuma za Urusi.
Kupitishwa kwa sheria hiyo na bunge la congress kutamnyima uwezo Rais Trump, kuondoa kikwazo chochote kitakachopitishwa dhidi ya Urusi.
Urusi imeendelea kupinda shutuma za kuingilia uchaguzi huo.
CHANZO-BBC SWAHIL
Social Plugin