Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania imesema imesikitishwa na matamshi ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema imesikitishwa na kauli ya rais wa awamu ya tatu akirudia maneno ya kejeli ya watanzania wenye maoni tofauti.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Mkapa alisema akiwa Chato, Geita kuwa Takwimu zilizotolewa na Waziri wa Afya siku hiyo( Julai 10, 2017) ya makabidhiano ya nyumba 50 zilizojengwa na Mkapa Foundaton Zitawasaida kupunguza Upumbavu Wale aliowaita hivyo Wakati wa Kampeni 2015.
Taarifa hiyo imesema kuwa matamshi ya Mkapa hayapendezi kusikika yakitoka kwa kiongozi wa kitaifa, na ni matamshi yasiyoheshimu maoni tofauti.
==>Isome taarifa hiyo hapo chini