USAJILI SIMBA, YANGA WAZUA UTATA


Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limezikumbusha klabu zote ambazo zinasimamiwa na shirikisho hilo kuhakikisha zinamaliza zoezi lake la usajili mapema.


TFF imetoa tamko hilo kupitia kwa Ofisa Habari, Alfred Lucas kuwa katika timu 16 za Ligi Kuu ya Tanzania Bara ni mbili pekee ndizo ambazo zimewasilisha majina yao ya usajili kuelekea msimu ujao wa 2017/18.

Katika majina ya klabu hizo, Simba na Yanga siyo miongoni mwao, hiyo inamaana kuwa kumbe hata wachezaji wao wapya waliosajiliwa hivi karibuni bado hawatambuliki ndani ya mfumo wa usajili wa shirikisho hilo.

Baadhi ya wachezaji waliosajiliwa hivi karibuni ni Emmanuel Okwi kwa upande wa Simba na Ibrahim Ajibu upande wa Yanga.

Alfred amesema timu 24 za Ligi Daraja la Kwanza na 24 Ligi Daraja la Pili zinatakiwa kukamilisha mfumo wa usajili kwa kuwa imesalia wiki moja tu kabla ya mfumo kufungwa.

Dirisha la usajili lilifunguliwa Juni 15, mwaka huu na litarajia kufungwa Agosti 6, mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post