SERIKALI imetoa onyo kwa watumishi wa
umma wanaotoa siri za serikali na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii
kuwa watachukuliwa hatua za kisheria.
Onyo hilo lilitolewa jijini Dar es
Salaam jana na Waziri wa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Angella Kairuki (pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa
watumishi wa umma wa Manispaa ya Ubungo.
Kairuki alisema mtumishi wa umma
atayejihusisha na usambazaji wa taarifa za serikali, atachukuliwa hatua
za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani na kupewa kifungo cha miaka 20
jela. Alisema serikali ina utaratibu wake wa kutoa taarifa kwa umma
ikiwa ni pamoja na kupitia machapisho yake kwa jamii.
Social Plugin