Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama,wa pili kulia ambaye jana alipata fursa ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC),wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Anna Mghwira na wa kwanza kulia ni Meneja mkuu Kilimanjaro Machine Tools Eng.Adriano Nyaluke akitoa taarifa za uzalishaji wa kiwanda hicho(Picha na Pamela Mollel Arusha)
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama akiteta jambo na wakurugenzi wa mifuko ya jamii wakati wa ziara yake katika kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC),Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa GEPF Mh..Daud Msangi ,kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Pensheni wa PPF Mh. William Erio
Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa GEPF Mh.Daud Msangi akizungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho,alisema mfuko wa hifadhi ya jamii ya GEPF umeshakamilisha mkopo wa bilion 1.6 kwaajili ya kuboresha kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na kutengeneza kinu cha kuyeyushia vyuma,kukarabati mfumo wa umeme,pamoja na kununua malighafi.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Joakim Mhagam akiwa anatoa maelekezo katika kiwanda hicho ambapo alisema kuboreshwa kwa kiwanda hicho kitasaidia ajira kwa vijana.
Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Wizara ya viwanda,Biashara na Uwekezaji Eng.Elli Pallangyo akitoa ufafanuzi kwa Waziri.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagam akiangalia baadhi ya vyuma vilivyo zalishwa katika kiwanda hicho
Kaimu Mkurugenzi mwendeshaji shirikisho la Taifa Maendeleo (NDC)Mh.Ramson Mwilangali akitoa maelezo kwa Waziri.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho amabapo alisema anaunga mkono jitihada za serikali katika kufufua viwnda hapa nchini
Mashine za uzalishaji
Wa kwanza kushoto ni Joseph Mrina Ambaye ni kiongozi mkuu ndani ya kiwanda hicho akiwa na Anna Mosha ambaye yeye ni Fundi wa mashine wakionyesha moja ya mashine ya kuranda mbao waliyoitengeneza hivi karibuni
Wakurugenzi wa Key Media Arusha Sara Keiya na Anna Keiya wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama
Moja ya wafanyakazi katika kiwanda hicho akiendelea na uzalishaji
Katibu wa shirikisho la mifuko ya hifadhi ya jamii nchini (TSSA)Meshach Bandewa akitoa utambulisho kwa Waziri.
*****
Serikali ipo katika hatua za mwisho katika kuhidhinisha bilioni 1.6 kutoka katika mfuko wa hifadhi za jamii GEPF kwaajili ya kujenga kinu cha kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha kutengeneza
vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC)
Akizungumzajana katika kiwanda hicho mara baada ya kutembelea Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama,alisema kuwa fedha hizo zitatumika kwaajili ya kuboresha kiwanda hicho kwa lengo la kufufua kwa kuwa kiwanda hicho kinabeba dhana nzima ya maendeleo ya uchumi wa viwanda kwenye nchi ya Tanzania.
Alisema kuwa mfuko wa GEPF baada ya kupokea maagizo kutoka
kwa Rais akihimiza Serikali ya viwanda ,wameweza kujiridhisha kuwa wanauwezo wa kuwekeza katika kiwanda hicho cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools (KMTC)
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Pensheni wa GEPF Daud Msangi alisema kuwa katika uwekezaji huo kiwanda hicho kitaweza kujenga kinu cha kuyeyushia vyuma ambayo ndio malighafi yao kubwa ya kuchonga vipuri na mashine mabalimbali
Aidha aliongeza kuwa kiwanda hicho kinakabiliwa na chagamoto ya umeme ambapo pesa hizo zitatumika katika kukarabati mfumo wa umeme katika kiwanda hicho.