Majaliwa ametoa kauli hiyo leo (Julai 5,2017) alipohitimisha shughuli za mkutano wa saba wa Bunge la 11 mjini Dodoma.
Akizungumzia hali ya chakula nchini, Waziri Mkuu amesema bado kuna maeneo yenye upungufu wa chakula.
"Hali ya chakula si ya kuridhisha sana, bado kuna maeneo yenye upungufu wa chakula," amesema.
Majaliwa amesema hata hivyo, kuna maeneo yaliyopata mvua nyingi na chakula cha kutosha.
"Hii ni kutokana na mazao ya chakula kuanza kukomaa katika maeneo hayo. Pia, baadhi ya wakulima kuanza kuvuna mazao yao,” amesema.
Waziri Mkuu amesema kwa baadhi ya maeneo mazao ya chakula na hasa mahindi yameanza kushuka bei katika masoko.
Amesema licha ya upungufu wa chakula katika nchi zinazoizunguka Tanzania, Serikali imepiga marufuku usafirishaji wa mahindi nje ya nchi bila kibali.
Pia, ameagiza mazao kuongezwa thamani badala ya kusafirishwa yakiwa ghafi.
Social Plugin