WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AJIUNGA NA PSPF MAONESHO YA SABASABA 2017



Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (kulia), akikabidhiwa kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, muda mfupi baada ya Mhe. Waziri kujiunga na Mpango huo leo Julai 8, 2017, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, ambapo PSPF inatoa huduma zote kwenye Maonesho hayo.

Waziri Dkt. Mpango, (kulia), akimsikilzia kwa makini Bw. Njaidi kuhusu faida zitokanazo na kujiunga na Mpango wa PSS 
Waziri Dkt. Mpango(kulia), akipokea fomu ya kujiunga na PSS, kutoka wka Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msanii maarufu, Mrisho Mpoto. Katikati ni Afisa Habari Mwanamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Habari na Picha wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Rodney Thadeus, akiweka dole gumba kwenye fomu ya kujiunga na uanachama wa PSPF kupitia PSS, leo Julai 8, 2017

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango,(pichani) amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari na kuhimiza wananchi kufanya hivyo kwani moja ya faida kubwa ni kujihakikishia kuwa na bima ya Afya.


Waziri aliyasema hayo leo Julai 8, 2017, wakati alipotembelea banda la PSPF lililoko jengo la Wizara ya Fedha na
Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasaba wakati wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea.


“Mimi nitoe wito kwa wananchikujiunga zaidi na mpango huu kwani watafaidika na huduma ya afya na nyinyi muongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge zaidi”alisema Mhe.
Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango pia alikabidhiwa kadiyake ya uanachama muda mfupi baada ya kujiunga.

“Mheshimiwa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari una faida nyingi na tumewalenga hasa watu wa kawaida kama vile wajasiriamali, wakulima, mama lishe, bodaboda, namachinga, na tumekuwa tukipata watu wengi wanaokuja kujisajili na Mpango huu na
wengi wao wamevutiwa na hii Bima ya Afya ambayo ni moja ya faida azipatazomwananchama”,alisema Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati
akimkabidhi Mhe. Waziri akdi yake ya uanachama.

Bw. Njaidi pia alimwambia Mhe. Waziri kuwa, kwa kujiunga kwake na Mpango huo wa uchangiaji wa Hiari, kutasaidia pia kuwakadia bima ya afya wasaidizi wake katika miradi kama vile ya
shambani na ufugaji.

“ Hawa wote wanawezakuingia kwenyempango huu wa bima kupitia uanachama wako katika Mfuko” ,alimuhakikishia Mhe.
Waziri.
Waziri Mpango (kulia), akiuliza maswali kwa maafisa wa PSPF
Mwananchi akisoma kipeperushi chenye taarifa za PSPF alipotembelea banda la Mfuko huo leo Julai 8, 2017
Baada ya Mwanachi huyu kuelewa huduma za PSPF na faida zake kwake, hatimaye alikata shauri la kujiunga na Mpango wa PSS, kwa kujaza fomu kama picha hii inavyojieleza.
Waziri Dkt. Philip Mpango, (kulia), akipokea mkoba wenye vipeperushi vya taarifa mbalimbali za PSPF, kutoka kwa balozi wa Mfuko huo, Msanii maarufu Mrisho Mpoto baada ya kutembelea banda la Mfuko huo leo Julai 8, 2017
Mhandisi Ally Shanjirwa wa PSPF, akiwapatia maelezo wananchi hawa waliofika kutembelea banda la Mfuko huo
Bw.Noah Amri, (kulia), Afisa wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akizungumza na mwanchi huyu aliyeshika fomu ya kujiunga na Mpango huo
Maafisa wa PSPF wakiwa kazini.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post