Mfanyabiasha Ramadhani Athumani Juma maarufu kama Elias Jeremiah Mazimbaka amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kujitambulisha kuwa yeye ni Mkurugenzi wa Habari wa Ikulu, Gerson Msigwa.
Amesema hati ya mashtaka jana wakili wa Serikali, Jacqline Nyantori alidai kuwa kati ya Juni 28 na Julai 4,2017 Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya alijitambulisha kama Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Habari wa Ikulu kwa Ladslaus Matindi.
Amedai kuwa mshtakiwa huyo alifanya kosa hilo katika kipindi hicho kwa lengo la kujaribu kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu
Mshtakiwa alikana shtaka upande wa mashtaka ulidai upelezi bado haujakamilika, Mshtakiwa ametakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao watasaini bondi ya sh 1 milioni.Kesi imeahirishwa 23,8,2017 na mtuhumiwa hajakamilisha masharti hayo.
Social Plugin