BI. REHEMA JUMA ANAWAOMBA MSAADA WA KUPATA MATIBABU KUTOKANA NA UVIMBE UNAOMSUMBUA KWA TAKRIBANI MIAKA 17


Bi. Rehema Juma Kishena kama anavyoonekana pichani na uvimbe unaomsumbua kwa miaka 17 sasa.
Bi. Rehema Juma Kishena akiwa na mtoto wake wa ( 3) Sophia Dastan Mandia nyumbani kwa dada yake Levolosi mkoani Arusha.
Bi. Rehema Juma Kishena akiwa na mtoto wake Sophia Dastan Mandia pamoja na dada yake bi Aziza Bakari Muyai nyumbani kwake Levolosi Mkoani Arusha.

Na Vero Ignatus, Arusha.

Mwanamke mmoja mkazi wa Levolosi Arusha bi Rehema Juma Kishena (40) anawaomba watanzania wenye mapenzi mema kumsaidia kupata fedha ya matibabu kutokana na tatizo la uvimbe linalomsumbua katika shavu lake la kulia ambalo limezunguka takribani robo tatu ya uso wake .

Mwanamke huyo ambae ni mama wa watoto (4) amesema kuwa tatizo hilo lilimuanza kwa jino kuumua ,akachukua hatua ya kwenda hospitalini kuling’oa , mwaka 2001 uvimbe ulijitokeza katika jino alilong’olewa, na kupelekea kufanyiwa upasuaji, baada ya miaka mitatu uvimbe ulirudi tena kama awali.


‘’Jino lilikuwa linaniuma nikaenda hospitalini kuling’oa, ndipo ukaanza uvimbe kwenye jino nililongoa nikarudi hospitalini wakaniambia nifanyiwe upasuaji ili kuondoa uvimbe ,baada ya miaka mitatu tatizo hilo likajirudia kama lilivyokuwa mwanzo “alisema Bi. Rehema.

Amesema kuwa kwa sasa hana msaada wowote kwani wazazi wake ni wazee, hawana mwezo wa kumsaidia,yeye mwenyewe hana mume kwani alimkimbia wati alipoona tatizo linaendelea kuwa kubwa.

“Nawaombeni msaada ili niweze kujitibu kwani hali yangu kama mnavyoiona nipo kwa dada yangu hapa ,sina msaada wowote” alisema Bi. Rehema.

Kwa upande wake dada yake (Rehema)Aziza Bakari Muyai amewaomba watanzania kushirikiana nae katika kumsaidia mdogo wake ili aweze kupatiwa matibabu kwani hali yake inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyozidi kwenda.

Ameomba kwa yeyote aliyepo tayari kumsaidia atumie mawasiliano kwa namba 0653179373.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post