Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BIBI HARUSI AJARIBU KUMUUA MUME WAKE SAA CHACHE BAADA YA KUFUNGA NDOA


Bibi harusi katika jimbo la Tennessee nchini Marekani ametiwa nguvuni baada ya polisi kusema kuwa alitoa bunduki kwenye gauni lake la harusi na kumtishia mumewe saa chache tu baada ya kufunga ndoa.

Kate Elizabeth Prichard, mwenye umri wamiaka 25, alikuwa bado amevalia gauni la harusi wakati alipokamatwa katika hoteli moja katika mji wa Murfreesboro.

Alidaiwa kuchukua bunduki aina ya pistol, na kuiweka kwenye kichwa cha mumewe na kufyatua.

Bunduki haikuwa na risasi ,lakini baadae alidaiwa kuijaza risasi na kufyatua angani, jambo lililowafanya waliokuwa wakishuhudia tukio hilo kukimbia.

Walioshuhudia tukio hilo waliandikisha taarifa kwa polisi ndipo polisi walipowasili eneo la tukio.

Walisema wawili hao walikuwa wakinywa pombe nje ya hoteli.

Sajenti polisi katika mji wa Murfreesboro Kyle Evans alisema kuwa maharusi hao wote wawili hawakushirikiana na mamlaka.

"Alivuta pistol kutoka kwenye gauni lake la harusi," Sajenti Evans aliviambia vyombo vya habari vya eneo hilo.

"akaielekeza kwenye kichwa cha mume wake na kufyatua.

" Maafisa walimfahamisha mumewe afahamu kwamba fungate imeisha na mkewe mpya anakwenda jela ." aliongeza Sajenti Evans

Sajenti Evans alisema kuwa bibi harusi alijaribu kuficha silaha bafuni katika hoteli walimokuwa.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com