Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya,Wilson Nkhambaku.
***
Chama
cha mapinduzi mkoa wa Mbeya kimetoa pole kwa wafanyabiashara waliopoteza
mali zao kufuatia janga la moto ulioteketeza soko la SIDO Agosti 15,2017.
Akitoa taarifa ya chama hicho kwa waandishi wa habari,leo Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya,Wilson Nkhambaku, alisema Chama Cha Mapinduzi kimeelezea masikitiko yake kutokana na kuungua kwa soko-tegemeo
la SIDO.
"Tukio hili si tu limewaumiza na kuwasononesha wafanyabiashara
wa SIDO, bali limekiumiza Chama chetu Cha Mapinduzi, serikali, taasisi,
mbalimbali na wananchi wote kwa ujumla" ,alisema Nkhambaku.
Alisema athari za kuungua moto soko la SIDO ni kubwa kiuchumi,
kiusalama, kijamii na kisaikolojia.
"Wapo
wafanyabiashara waliokuwa na mikopo kwenye mabenki na taasisi nyingine za
kifedha ambao sasa watakuwa na wakati mgumu kurejesha mikopo yao, ni
kwa msingi huo Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya kinaungana na taasisi zingine
kuwapa pole sana wafanyabiara ambao mali zao zimeteketea kwa moto",alieleza.
Aidha, alisema Chama Cha Mapinduzi kupitia kwa wabunge wake mkoani Mbeya, na hasa mbunge wa
viti maalum Dr. Mary Mwanjelwa, wote wametuma salamu nyingi za pole kwa
wafanyabiashara na wajasiriamali ambao wamepoteza mali zao.
Nkhambaku alisema kufuatia tukio hilo Chama Cha Mapinduzi kimeshaiagiza serikali ya mkoa kuunda
tume ya uchunguzi ili kuweza kubaini nini chanzo cha moto huo na pia hasara
iliyotokana na janga hilo.
"Chama
kimeielekeza serikali kuhakikisha kwamba tume hiyo inafanya kazi kwa umakini,
uadilifu na ndani ya siku tano kuanzia tarehe 16-21/8/2017 iwe imeshakamilisha
kazi hiyo na kutoa taarifa",alieleza Nkhambaku.
Alisema tayari tume ya watu 9 imeshaundwa
na iko kazini kufuatilia suala hilo.
Alisema Chama
cha mapinduzi kimetoa wito kwa wafanyabiashara walioathirika na janga hilo na
wananchi wote wa Mbeya kikiwasihi sana waendelee kuwa watulivu katika
kipindi hiki kigumu wakati serikali ikishughulikia jambo hilo.
Aidha alisema CCM alihahakikishia wananchi wote kwamba ckipo pamoja nao katika
wakati huu mgumu unaowakabili na kwamba chama kitashirikiana nao hadi ufumbuzi wa
kudumu utakapopatikana.
Imeandikwa na Mwandishi wetu-Mbeya
Social Plugin