Juzi usiku, mwanamuziki Diamond Platnumz na kundi zima la wasanii wa WCB wametoa wimbo “Zilipendwa”, ukionekana kuwa mkakati wa kukabiliana na kibao kipya cha msanii anayeaminika kuwa ni hasimu wake mkuu, Ali Kiba, ambaye mchana wa siku hiyo aliachia wimbo wa “Seduce Me”.
Diamond na kundi lake walitoa wimbo saa 12 tu tangu Ali Kiba aachie wake, hali ambayo imetafsiriwa kuwa ni kutaka kuudhibiti wimbo wa “Seduce Me”.
Katika wimbo “Zilipendwa”, Diamond Platnumz ameshirikiana na wasanii wote wa WCB, ambao ni Harmonize, Rayvanny, Queen Darlin, Rich Mavoko, Lavalava na Marombosso.
Kitendo cha Diamond kutoa wimbo mpya kimetafsiriwa kama umoja unaoshindana na Alikiba, huku mashabiki wakifananisha na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao ulianzishwa na upinzani dhidi ya CCM wakati wa Bunge Maalumu la Katiba.
Wengine wamekuwa wakituma vibonzo vinavyomuonyesha tembo akishambuliwa na simba wengi.
Kuthibitisha kuwa wimbo huo umetolewa kama mashindano, Babu Tale, mmoja wa mameneja wa Diamond Platnumz, ameandika katika akaunti yake ya Instagram akisema: “Tushindane kwenye kazi, vya mitandao tuwaachie mashabiki”.
Kauli hiyo imetolewa baada ya kuwepo malumbano katika mitandao ya kijamii yanayowahusisha Diamond, Ali Kiba na Ommy Dimpoz. Hata hivyo, kauli za wasanii hao katika siku za karibuni zinapingana na majibu ambayo wamekuwa wakitoa muda mrefu kwamba hawana uhasimu isipokuwa ni mashabiki ambao wanawagombanisha kwa kuwashindanisha.
Kutoa kazi ndani ya saa 12 baada ya kazi nyingine, inaonyesha wazi kuna tatizo.
Katika siku za hivi karibuni WCB imekuwa ikitoa kazi mfululizo. Kazi hizo zisizopongua 13 ni kama “Zezeta” na “Mbeleko” za Rayvanny, pamoja na “Sheri”, “Mpe Habari” na “Wanakutamani” za Rich Mavoko. Pia “Happy Birthday”, “Show Me”, “Niambie” na “Sina” (Harmonize), “Dede” na “Teja” (Lavalava), huku Diamond akitoa “Eneka”, “Fire” na “I Miss You”.
Chanzo-Mwananchi
Chanzo-Mwananchi
Social Plugin