Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT. KALEMANI AITAKA TANESCO KUUNGANISHA NGUVU KUKAMILISHA MIRADI YA UMEME YA KURASINI NA KIMBIJI



NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani,(pichani anayeongea), amelitaka Shirika la Umeme
Tanzania TANESCO kuunganisha nguvu ili kuhakikisha wanakamilisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusamabaza umeme kinachotarajiwa kujengwa huko
Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kalemani ametoa maelekezo hayo Agosti 22, 2017, wakati alipofanya ziara kukagua miradi ya umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini, Kigamboni na eneo panapotarajiwa kujengwa kituo kingine cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.

“Hakikisheni mradi wa ujenzi wa kituo hiki cha Kimbiji unakamilika ifikapo Machi 30, mwakani,(2018), na kuwaondolea adha ya upatikanaji wa umeme wananchi wa Kigamboni, chukueni mafundi waliokamilisha kazi ya kujenga kituo cha umeme kule Mtwara waje hapa, muwaache wale wanaojenga transition (njia ya kusafirisha umeme) wajenge, lakini wale mafundi wengine waleteni hapa ili mradi huu ukamilike”,alifafanua.

Akiwa kwenye kituo cha kupoza na kusamabza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam, Dkt. Kalemani aliipongeza TANESCO kwa juhudi kubwa walizofanya kwa hatua ujenzi waliyofikia ambapo sasa wameanza kufunga mashine kubwa. Kituo cha Kurasini ndicho kinachotegemewa sana na watu wa Mbagala, Kurasini na Kigamboni.

Ongezeko la haraka la wakazi kwenye maeneo ya Mbagala, na Kigamboni kumepelekea uhitaji mkubwa wa umeme ambapo umeme unaopatikana kwa sasa umekuwa haukidhi mahitaji ya wakazi wa maeneo hayo.

“Naomba niwaambie, mradi huu umechelewa sana, hivyo basi ongezeni kasi ili ifikapo Agosti 30, mwaka huu,
mradi ukamilike nataka watu wa Mbagala, watu wa Kurasini, na watu wa Kigamboni wanaondokana na kero hii ya umeme, na mimi nitawaambia washeshimiwa wabunge wa
Kigamboni Mheshimiwa Ndungulile (Dkt. Faustin Ndungulile) na Mheshimiwa Mangungu (Murtaza Magungu) Mbunge wa Mbagala kuhusu habari hii ili wawaambie
wananchi wa maeneo haya wawe wavumilivu kwani mradi huu sasa utakamilika”,alisema.


Dkt. Kalemani pia aliwaagiza viongozi wa TANESCO, kuhakikisha wanakusanya nguvu kwa maana ya vifaa kutoka ofisi zote za TANESCO mkoa wa Dar es Salaam, ili
kuhakikisha wananchi wote wa Kigamboni wanaofikia 350 waliolipia ada za kuunganishiwa umeme wawe wamepelekewe umeme ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Agosti.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka,aliwaambia waandishi wa habari kuwa maelekezo ya Mheshimiwa Naibu waziri
yatafanyiwa kazi kwa haraka ili kuhakikisha kero hiyo inaondoka.
Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James,(kulia), akimpatia maelezo Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme Kurasini jijini Dar es Salaam.Picha zote na K-VIS BLOG/Khalfan Said
Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid  James,(kulia), akimpatia maelezo Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kituo 
cha kupoza na kusambaza umeme Kurasin jijini Dar es Salaam
Dkt. Kalemani (katikati), akitoa maagizo kwa wakandarasi wanaotekeleza mradi huo wa Kurasini. 
Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es
Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (watatu kushoto), akimpatia maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha umeme cha Kigamboni, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wa pili kushoto)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (kulia), akiwa na Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid  James, (kushoto), akiongea na waandishi wa habari.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Jahulula akifafanua baadhi ya mambo kwenye eneo ambalo patajengwa kituo cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji, Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani
Meneja wa TANESCO Mkoa
wa Temeke, Mhandisi Jahulula, (wapili kulia), akifafanua baadhi ya mambo kwenye eneo ambalo  patajengwa kituo cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji, Kigamboni 
jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na  Madini, Dkt. Medard Kalemani(katikati).
Fundi wa TANESCO akiwa kazini pale Kigamboni
Mhandisi Jahulula, (kushoto), akionyesha mahala mpaka wa eneo hilo la mradi unapoishia. 
Dkt. Kalemani (katikati), na viongozi wa TANESCO wakiwa kwenye eneo hilo la Kimbiji
Picha zote na K-VIS BLOG/Khalfan Said

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com