Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JINSI SOKO KUU LA MBEYA 'SIDO' LILIVYOTEKETEA KWA MOTO


Soko kuu la Jijini Mbeya maarufu kama SIDO limeungua moto usiku wa kuamkia leo .Moto huo ulianza majira ya saa 3 usiku ambapo mali za wafanyabiashara mbalimbali katika soko hilo zimeteketea.

Kwa upande mwingine wananchi wamesikika wakimwaga machozi ya lawama kwa Jeshi la Polisi wakilaumu kutoruhusiwa kusogea eneo la tukio kuokoa mali zao kwa kuwafyatulia risasi hewani.

Hii ni mara ya tatu sasa ambapo soko hili liliisha ungua mara mbili mfululizo kabla ya kuungua tena kwa mara nyingine usiku wa kuamkia leo.


Tazama video ya tukio hilo hapo chini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com