Upande wa Mashtaka katika kesi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’ leo umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamekusanya nyaraka za upelelezi na zimepelekwa kwa mtaalamu wa maandishi.
Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali, Estazia Willson mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.
Wakili Wilson amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, pia wamekusanya nyaraka na zimepelekwa kwa mtaalam wa maandishi, hivyo wanasubiri ripoti.
Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi September 8, 2017.
Social Plugin