Korea Kaskazini inasema mpango wake ya kufyatua makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam, utakuwa tayari hivi karibuni huku majibizano ya kivita kati yake na Marekani yakiendelea.
Vyombo vya habari vilisema kuwa makombora ya Hwasong-12 yatapita anga ya Japan na kuanguka baharini karibu kilomita 30 kutoka kisiwa cha Guam ikiwa mpango huo utaidhinishwa na Kim Jong-un.
Korea ilipuuzna onyo la Donald Trump kuwa itashambuliwa vikali.
Marekanai imeionya Korea Kaskazini ikisema kuwa vitendo vyake vinamaanisha kuwa huo utakuwa mwisho wa utawala wa nchi hiyo.
Waziri wa ulinzi nchini Marekani Jim Mattis alisema kuwa Korea Kaskazini itapigwa vibaya ikiwa itaingia vitani na Marekani na washirika wake.
Korea Kaskazini ilitangaza siku ya Jumatono kuwa inachora mipango ya kufanya mashambulizi ya makombora katika kisiwa kilicho bahari ya Pacific cha Guam kilicho na kambi za jeshi la Marekani na watu 163,000
Taarifa iliyotolewa baadaye ilisema kuwa jeshi litakamisha mpango huo ifikapo katikati mwa mwezi Agosti na kupeleka kwa kiongozi wao Kim Jong-un kuidhinishwa.
Social Plugin