Mwili wa Nyanda Madirisha ukiwa chini baada ya kupata ajali ya pikipiki na kufariki dunia huko Maswa mkoani Simiyu Agosti 06,2016
Waombolezaji wakiwa wabeba jeneza lililobeba mwili wa Nyanda Madirisha tarehe 07.08.2016 wakati wa mazishi
Mrithi wa Nyanda Madirisha 'Nchaina' huyu ndiyo alikabidhiwa rasmi na ukoo mikoba ya Nyanda Madirisha ikiwa ni pamoja na vitendea kazi na wanenguaji
Maliganya 'Nyanda Madirisha Wabhado' anayefanana sana na marehemu Nyanda Madirisha
********
Leo Agosti 06,2017 Wapenzi wa Nyimbo za asili na mashabiki wa Msanii Maarufu wa Nyimbo za asili Nyanda Madirisha ‘The Super Star’ wanakumbuka siku ya kifo chake siku ya Jumamosi tarehe 06.08.2016 mchana akijiandaa Kufanya Show huko Maswa mkoani Simiyu.Soma Zaidi <HAPA>Kuhusu Kifo Cha Nyanda Madirisha.
Baada ya kifo chake,Wadogo zake na Marehemu Nyanda Madirisha ambao ni Nyanda Maliganya na Nyanda Nchaina waliamua kurithi kazi ya kaka yao wakitumia mitindo mbalimbali iliyokuwa inatumiwa na Kaka yao.
Akizungumza na Malunde1 blog leo Jumapili Agosti 06,2017,Mrithi wa Nyanda Madirisha "Nchaina" ambaye alikabidhiwa na ukoo mikoba ya kaka yake ikiwemo vitendea kazi na wanenguaji,amesema ameamua kusitisha show alizokuwa anaendelea nazo katika mikoa mbalimbali nchini ili kuomboleza kifo cha kaka yake kipenzi.
"Tumekusanyika hapa nyumbani katika kijiji cha Shunu kata ya Nyahanga tarafa ya Hongwa wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kumuenzi na kuomboleza kifo cha kaka yangu kipenzi Nyanda Madirisha,siku hii inaniumiza sana,tulifanya kazi naye,alinifunza mambo mengi ya maana lakini leo siko nae,Namuomba Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,amina",amesema Nchaina.
Amesema miongoni mwa shughuli zilizofanyika wakati wa maombolezo hayo ni kupiga nyimbo mbalimbali za marehemu huku wakiiga mambo mbalimbali yaliyokuwa yanafanywa na Nyanda Madirisha enzi za uhai wake.

Malunde1 blog inakualika Kutazama Ngoma za wadogo zake Nyanda Madirisha (Maliganya na Nchaina),Ngoma za Marehemu Nyanda Madirisha, mazishi ya Nyanda Madirisha na Video kukanusha uvumi wa Kufufuka kwa Nyanda Madirisha.
ZITAZAME HAPA CHINI
Nchaina- Biashara
Nchaina- Biashara
Nchaina- Nalisosomeje
Nchaina Rambirambi
Nchaina -Bhalomolomo
Maliganya-Hela Yabhulaga Bhudugu
Maliganya-Yamuwelelo
Maliganya- Wayela
Nchaina ft Maliganya- Kifo cha Nyanda Madirisha
Mazishi ya Nyanda Madirisha
Uzushi Kufufuka Nyanda Madirisha
Nyanda Madirisha - Matukio
Nyanda Madirisha - Shikolo
Nyanda Madirisha- Magong'ho ( Wimbo aliojitabiria kifo)
Nyanda Madirisha ft Ng'wana Mazuri
Social Plugin