Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Live : MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA UCHAGUZI MKUU KENYA LEO AGOSTI 8,2017



Kwa mara nyingine tena, Uhuru Kenyatta na Raila Odinga, wanashindania uongozi wa taifa la Kenya baada ya kukabiliana tena Machi 2013.

Rais Kenyatta ni mwana wa rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta naye Bw Odinga mwana wa makamu wa rais wa kwanza Jaramogi Oginga Odinga.

Familia hizo zilianza kwa kuwa marafiki wa kufa kuzikana wakati wa Kenya kujipatia uhuru wake. Jaramogi alipewa fursa ya kuwa kiongozi wa kwanza wa Kenya na Waingereza lakini akaikataa fursa hiyo na kusema Kenya haiwezi kupokea uhuru kiongozi wake Mzee Kenyatta akiwa jela.

Jomo Kenyatta aliachiliwa na akawa waziri mkuu na mwaka mmoja baadaye baada ya Kenya kuwa jamhuri akawa rais wa kwanza wa Kenya, na Jaramogi akawa makamu wake.

Lakini uhasama ulizuka mwaka 1966 na Kenyatta akamfuta kazi Jaramogi na kuanzia hapo uhasama wa muda mrefu kati ya jamii ya Wakikuyu (Kenyatta) na Wajaluo (Odinga) ukaanza.

Uhuru Kenyatta na Odinga walishindana katika uchaguzi wa urais mwaka 2013 na Bw Kenyatta akaibuka mshindi.

Wakati huu, kivumbi tena ni kati ya wawili hao.

Bw Odinga anagombea urais mara ya nne na ushindani kati ya wawili hao ni kama umefikia kilele.

Raia wa Kisumu akionesha kidole baada ya kupiga kura

Raia wakipiga kura kituo cha Wabungo, Kwale pwani ya Kenya


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com