Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MADIWANI WATATU WA CHADEMA WAJIUZULU NAFASI ZAO

Madiwani watatu wa Chadema Manispaa ya Iringa wameamua kuachia nafasi zao kwa madai ya mwenendo mbaya wa chama.

Madiwani hao walichukua uamuzi huo baada ya kumwandikia barua ya kujiuzulu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa. Madiwani ambao wamechukua uamuzi huo ni Baraka Kimata wa Kata ya Kitwiru na wawili wa viti maalumu; Husna Ngasi na Leah Mlelewa.

Wakizungumzia uamuzi huo, viongozi hao walisema kuwa wameamua kufanya hivyo baada ya kuchoshwa na mwenendo wa chama hicho.

Kimata alisema anaendelea na kazi zake nje ya siasa na kwamba, hatabaki na nafasi yoyote ndani ya chama hicho.

Alisema kuwa ushirikiano mdogo kati yake na mbunge wa jimbo hilo umemsukuma kuachia nafasi yake hiyo.

Kwa upande wake, diwani mwingine ambaye alikuwa katibu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Mlelewa alisema hatabaki na nafasi yoyote ndani ya chama hicho kama ilivyo kwa Kimata.

Madiwani wengine wa Chadema ambao walijiuzulu kutoka Jimbo la Arumeru Mashariki ni Anderson Sikawa, Emmanuel Mollel, Greyson Isangya na Josephine Mshiu pamoja na diwani wa Murieti, Credo Kifukwe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com