Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 25, 2017 imesema Mfanyabiashara Yusuf Manji ana kesi ya kujibu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha, wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi.
Hakimu Mkeha alisema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka na kwamba mshtakiwa ana haki ya kujitetea kutokana na mkojo wake kukutwa na dawa aina ya Morphine ambayo zao lake ni Heroin.
“Hivyo mshtakiwa anapaswa kujitetea kwa sababu Mahakama imemkuta na hatia,”
Baada ya kueleza hayo, Wakili wa utetezi Hudson Ndusyepo alidai kuwa mshtakiwa atajitete kwa hati ya kiapo ambapo watakuwa na mashaidi 15.
Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi August 30 Na 31, 2017 ambapo itasikikizwa mfululizo.
Social Plugin