Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu umetoa msaada wa magodoro 14 katika kituo cha afya Chela kilichopo katika Halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika wodi za wagonjwa katika kituo hicho.
Akizungumza jana Agosti 22,2017 wakati akikabidhi magodoro hayo, Kaimu Meneja wa Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Bryson Tarimo(aliyesimama pichani) alisema magodoro hayo 14 ni kwa ajili ya wodi za wagonjwa katika hicho cha afya.
"Afya ni haki ya kila mwananchi, katika juhudi za kuchangia uboreshaji wa huduma za afya kwenye halmashauri ya Msalala,kama wadau wa sekta ya afya, mgodi wetu umefika katika kituo cha Chela kwa mara nyingine tena kukabidhi magodoro haya ambayo tuliyoombwa mwaka huu wakati wa uzinduzi wa jengo la upasuaji ambalo pia tusishiriki ujenzi wake kupitia taasisi ya Mkapa Foundation",alieleza Tarimo
Akipokea magodoro hayo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dk. Hamad Nyembea aliushukuru mgodi huo kwa kutimiza ahadi yake ambayo waliitoa kwa Mkuu wa Mkoa wakati wadau wa sekta ya afya Msalala walipokabidhi jengo la upasuaji.
Kulia ni Kaimu Meneja wa Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Bryson Tarimo akishikana mkono na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dk. Hamad Nyembea wakati wa kukabidhi magodoro 13 kwa ajili ya kituo cha afya Chela
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dk. Hamad Nyembea akizungumza wakati wa kupokea magodoro hayo 14 yaliyotolewa na mgodi wa Bulyanhulu
Social Plugin