MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Nyakoro Sirro amefanya mabadiliko ya makamanda wa polisi mikoani.

Taarifa ambayo imetolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi   Barnabas Mwakalukwa  imesema kwamba  Sirro amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Juma Yusuf Ally kuwa Kaimu Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Uteuzi huo unafuatia kustaafu kwa aliyekuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdani Omari Makame kwa mujibu wa sheria baada ya kutimiza umri wa miaka sitini (60).

Kabla ya uteuzi huo DCP Juma alikuwa ni Mkuu wa Utawala na Fedha Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.

IGP Sirro pia amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi  (SACP) Lazaro Mambosasa kuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huo, SACP Mambosasa alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi  (SACP) Neema Mwalimu Mwanga anakwenda Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.

IGP Sirro pia amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Gilles Bilabaye Mroto kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na  Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Emmanuel Lukula kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke.

Kabla ya uteuzi huo, ACP Lukula alikuwa Ofisa Mnadhimu wa Polisi mkoa wa Mbeya.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote kuendela kushirikiana na Jeshi hilo kwa kufichua taarifa za uhalifu na wahalifu ili kwa pamoja tuendelee kuiweka Tanzania salama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post