Vijana 230 kutoka halmashauri za wilaya ya Kishapu na Manispaa ya Shinyanga wamekutana katika bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Bonanza hilo limefadhiliwa na Mfuko wa Kusaidia watoto wa Uingereza ( Children’s Investment Fund Foundation UK- (CIFF) limefanyika Jumamosi Agosti 12,2017 katika uwanja wa shule ya msingi Kolandoto kata ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga.
Miongoni mwa michezo iliyochezwa na vijana hao ni pamoja mpira wa miguu,kuvuta kamba,mbio za magunia,kukimbiza kuku ,kuimba mashairi,kucheza muziki na kuonesha fasheni za mavazi ambapo washindi walipatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo kombe na mabegi ya shule.
Akizungumza katika bonanza hilo mgeni rasmi Afisa Tabibu wa hospitali ya Kolandoto,Maryciana Bruno alisema lengo la bonanza hilo kwa ajili ya vijana kufurahi,kufahamiana,kupata marafiki wapya,kuonyesha vipaji na kujifunza.
“Bonanza hili limejumuisha vijana wenye umri wa kati ya miaka 14-19 wanaotoka katika klabu za vijana ambazo zimeundwa na zinasimamiwa na AGPAHI kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya vijana hawa wanatoka kwenye vikundi 10 vilivyopo katika halmashauri za wilaya mbili za mkoa wa Shinyanga ambazo ni Kishapu,Manispaa ya Shinyanga”,alieleza Bruno.
“Nalishukuru sana shirika la AGPAHI kuendelea kuwa karibu na vijana hawa wanaopata huduma kwenye vituo vya tiba na matunzo”,aliongeza.
Aidha aliwataka viongozi wa halmashauri za wilaya kuendelea kutoa ushirikiano kwa shirika hilo hususani katika kutekeleza majukumu ya kuwasaidia wananchi katika huduma za afya hususani kwa watu wanaopata tiba na matunzo ili huduma zipatikane katika ubora na ziwe rafiki kwa wananchi.
Naye Afisa Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simon Haule aliwashukuru wazazi na walezi wa watoto na vijana kuendelea kushirikiana na AGPAHI kwa ukaribu zaidi huku akiiomba serikali kuendelea kulipa ushirikiano shirika hilo ili kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi yanafanikiwa zaidi.
Kwa upande wake Mlezi wa Vijana rika ambaye pia ni Afisa Muuguzi Msaidizi katika kituo cha afya Kambarage Glory Assey alisema mafanikio ya AGPAHI yanatokana na uwepo wa huduma rafiki zinazotolewa kwa watoto na vijana.
Nao vijana walioshiriki bonanza hilo walilishukuru shirika la AGPAHI kwa kuwathamini,kuwajali watoto na kuwapatia huduma muhimu.
ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Afisa Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simon akitoa maelekezo kabla ya kuanza kwa bonanza la michezo kwa vijana 230 kutoka halmashauri ya manispaa ya Shinyanga na Kishapu.
Afisa Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simon akizungumza.
Vijana wakimskiliza Afisa Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga Charles Simon.
Mgeni rasmi,Afisa Tabibu wa hospitali ya Kolandoto,Maryciana Bruno akifungua bonanza la michezo kwa vijana hao.
Vijana wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa bonanza kutoka kwa mgeni rasmi.
Afisa Tabibu wa hospitali ya Kolandoto,Maryciana Bruno akizungumza wakati wa kufungua bonanza hilo.
Wa kwanza kushoto ni muuguzi kutoka hospitali ya Kolandoto,Grace Makungu,katikati ni Afisa Tabibu wa hospitali ya Kolandoto,Maryciana Bruno akifuatiwa na Mtunza takwimu za HIV hospitali ya Mwadui,Sweetbetty Majula.
Mlezi wa Vijana rika ambaye pia ni Afisa Muuguzi Msaidizi katika kituo cha afya Kambarage Glory Assey,akizungumza wakati wa bonanza hilo.
Mchezo wa kukimbiza kuku ukiendelea kwa upande wa vijana wa kike ambapo mshindi aliondoka na kuku huyo kama zawadi yake.
Mshindi wa mchezo wa kukimbiza kuku akiwa ameshikilia kuku wake wa ushindi.
Mchezo wa kuvuta kamba ukiendelea.
Mchezo wa kuvuta kamba.
Mlezi wa Vijana rika ambaye pia ni Afisa Muuguzi Msaidizi katika kituo cha afya Kambarage Glory Assey akitoa maelekezo kwa vijana namna ya kucheza mchezo wa kukimbia na mayai yaliyowekwa kwenye vijiko.
Vijana wakicheza mchezo wa kukimbia na mayai yaliyowekwa kwenye vijiko.
Mbio za kwenye magunia nazo zilikuwepo.
Vijana wakichuana mbio za kwenye magunia.
Vijana wakijiandaa kutimua mbio za mita 100.
Mshindi wa mbio za mita 100 kwa upande wa vijana wa kike akifurahia wakati wa kumaliza mbio hizo.
Vijana wa kiume wakikimbia mbio za mita 100.
Wachezaji wa timu ya mpira ya hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakijiandaa na mchezo dhidi yao na timu ya kituo cha afya Kambarage.
Wachezaji wa timu ya mpira ya kituo cha afya Kambarage wakijiandaa na mchezo.
Mchezo kati ya timu ya hospitali ya mkoa wa Shinyanga na kituo cha afya Kambarage ukiendelea.
Tunashangilia mpira wa miguu.....
Hadi mwisho wa mchezo, timu ya Kambarage iliibuka kidedea kwa kuichapa bao 5- 4 timu ya hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Vijana wakicheza muziki.
Burudani inaendelea.
Kijana akiimba shairi.
Vijana wakiimba shairi.
Burudani ya muziki ikiendelea.
Vijana wakionesha fashion za mavazi.
Vijana walioonesha fashion za mavazi wakiwa katika pozi.
Mlezi wa Vijana rika ambaye pia ni Afisa Muuguzi Msaidizi katika kituo cha afya Kambarage Glory Assey akitoa utaratibu wa utoaji zawadi kwa washindi wa michezo mbalimbali.
Mshindi wa mchezo wa kukimbiza kuku akishikana mkono na Mgeni rasmi,Afisa Tabibu wa hospitali ya Kolandoto,Maryciana Bruno.
Mshindi wa mbio za kwenye magunia upande wa vijana wa kiume akipokea zawadi ya begi la shule.
Mshindi wa mchezo wa kukimbia na mayai akipokea zawadi ya begi la shule.
Mshindi wa mbio za mita 100 upande wa vijana wa kike akijiandaa kupokea zawadi ya begi.
Mshindi wa mbio za mita 100 upande wa vijana wa kiume akipokea zawadi ya begi.
Mwimbaji bora wa shairi akipokea zawadi ya begi.
Mwakilishi wa kundi la wachezaji wa muziki akishikana mkono na Mtunza takwimu za HIV hospitali ya Mwadui,Sweetbetty Majula.
Kocha wa timu ya kituo cha afya Kambarage akipokea zawadi ya kombe
Vijana wa Kambarage wakifurahia kombe lao la ushindi.
Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog