Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha: RAIS WA SIMBA SC, EVANS AVEVA NA MAKAMU WAKE, GEOFREY NYANGE WAKIWA MAHAKAMANI

Leo August 7, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kwa mara nyingine kesi ya kutakatisha fedha na kughushi inayowakabili Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu hadi Agosti 16, 2017 baada ya upelelezi kutokamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mwambapa baada ya Wakili wa TAKUKURU, Kishenyi Mutalemwa kueleza kuwa upelelezi haujakamilika na kuomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com