Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kwamba imempa siku 7 Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu kuomba radhi kwa kupotosha umma.
Kwenye ukurasa wa twitter wa msemaji wa serikali ametoa taarifa akisema kuwa taarifa hizo si za kweli, kwani hata mtu aliyetumika kuandika hiyo taarifa yupo msibani.
"Umma unaarifiwa kuwa baada ya tamko la jana Serikali haijatoa tamko lolote tena.Uzushi unaosambazwa mitandaoni Jumapili hii ni wa kupuuzwa, taarifa inayosambazwa ni ya uongo kwa kuwa hata Dkt. Abbas anayetajwa kusaini bado yuko likizo ya kufiwa. Hatua kali zitachukuliwa", aliandika twitter ya Msemaji wa serikali.
Hapo awali kulikuwa na taarifa iliyosambaa ikionyesha imetoka serikalini, ikimtaka Mh. Tundu Lissu kuomba radhi huku ikimpa siku 7 tu za kufanya hivyo.
Social Plugin