Baada ya kambi ya muda mrefu ya club ya Simba nchini Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya wa Ligi na michuano ya kimataifa, Jumanne ya Agosti 8 2017 Simba Day, ilikuwa ni fursa kwa mashabiki wa timu yao kushuhudia utambulisho wa wachezaji wao wapya.
Simba ambao msimu huu wamefanya usajili wa zaidi ya wachezaji 10 wapya, siku ya leo Agosti 8 wamewatambulisha na kucheza mchezo wa kirafiki na Bingwa wa Rwanda Rayon Sports uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kushuhudia mastaa wapya kama Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi wakicheza game hiyo.
Haruna Niyonzima aliyeingia kipindi cha pili ndiyo mchezaji aliyekuwa kivutio zaidi kwa mashabiki baada ya kuihama Yanga ambao ndiyo wapinzani wa Simba msimu uliopita na katika historia, Haruna leo kaichezea Simba kwa mara ya kwanza katika maisha yake.
Game ya kirafiki ya Simba na Rayon imemalizika kwa Simba kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Mohamed Ibrahim dakika ya 16 kipindi cha kwanza, wakati Simba wanasubiria mchezo wa ngao ya hisani dhidi ya Yanga August 23, watacheza game ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar na Singida United.
Social Plugin