Klabu ya soka ya Stand United ya Shinyanga imebadili karibu kikosi chake chote kwa kusajili wachezaji wapya zaidi ya 18 na kubakiwa na wachezaji nane tu waliocheza kwenye msimu uliopita.
Katika kuhakikisha kikosi cha timu hiyo kinakuwa imara kwenye msimu mpya unaotarajiwa kuanza mwezi Septemba, ndani ya kundi hilo la wachezaji hao wapya wapo wanandinga watatu kutoka nje ya Tanzania.
Kwa mujibu wa katibu wa klabu hiyo, Kenedy Nyangi, amewataja wachezaji hao wa kigeni kuwa ni Steven Dua na David Mensa wote kutoka Ghana pamoja na Mzimbabwe Wisdom Mutesa ambaye amechukuliwa kwa mkopo akitokea Singida United.
Social Plugin