Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TIGO KUTOA SMARTPHONE ZENYE MUDA WA BURE WA MAONGEZI KILA SAA KWA SAA 24


Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, Wiliam Mpinga, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu promosheni mpya ya Jaza Ujazwe ambapo simu za kisasa 720 zitatolewa kila siku kwa washindi wa promosheni hiyo. Kulia ni Mtaalamu wa Bidhaa Mpya za Tigo, Jaqualine Nnunduma.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, Wiliam Mpinga, akionesha moja ya simu aina ya Teco S1 zitakazotolewa katika promosheni hiyo.
Mtaalamu wa Bidhaa Mpya za Tigo, Jaqualine Nnunduma, akizungumzia promosheni hiyo.
****

Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania, bado inawavutia wateja wake tena na prmosheni kubwa ambayo itashuhudia wateja hao wakiondoka na simu za mkononi za kisasa (Smartphones) kila saa kwa saa 24 kila siku. Simu za mkononi zitatolewa zikiwa na muda wa bure wa mawasiliano kwa mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa Tigo, jumla ya simu za kisasa (Smartphones) 720 zipo tayari kuchukuliwa katika kampeni ya promosheni hii mpya.

 Wateja wanaweza kushinda simu za mkononi kila saa tu kwa kuzijaza simu zao muda wa maongezi kwa kukwangua kadi, e-pin au TigoPesa, ambapo namba yao ya simu itaingia kwenye droo kwa ajili ya kushinda moja ya Smartphones za Tecno S1 ambayo itakuwa tayari kuchukuliwa kila saa, kila siku, katika siku saba za wiki.

Tofauti na promosheni nyingine ambapo ni wateja wachache tu wanapata zawadi chache, promosheni hii ya Tigo imethibitisha kusimama mahali ambapo kila mteja mmoja anazawadiwa kila anapojaza. Washindi wa Smartphone ya Tecno S1 watafurahia mawasiliano ya bure kwa mwaka mmoja ambapo zawadi nyingine za kushinda zinajumuisha bonasi ya bure katika sauti, data na ujumbe mfupi wa maneno ( SMS) kulingana na muundo wa matumizi wa wateja.

Akitangaza zawadi hizo mpya, Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema kuwa kampuni hiyo kwa mara nyingine tena imefurahishwa na mwitiko chanya wa wateja kwa kampeni maarufu ya Jaza Ujazwe na ndiyo sababu imewafanya waongeze zawadi za kuvutia zaidi pamoja na bonasi zaidi za kusisimua kama ishara ya shukrani.


"Ni sehemu ya utamaduni wa Tigo katika kutambua kuungwa mkono kusiko na ukomo ambao wateja wetu wametupa. Ndiyo maana, tunaamini kwamba wanastahili kupewa shukrani kwa kujitoa kwao kwa kwa ajili ya bidhaa na huduma zetu. Tuna furaha mara nyingine tena, kuwapatia wateja wetu zawadi hizi, zitakazowawezesha kuendelea kufurahia huduma zetu za maisha ya kidijitali ", alisema Mpinga.

Tuzo za kusisimua zinaendana na kuongezeka kwa miundombinu ya mtandao wa kisasa ya Tigo, aliongeza Mpinga akibainisha kuwa kipaumbele muhimu cha kampuni kilikuwa kikizingatia mahitaji ya wateja na kutoa suluhisho linalofaa kushughulikia mahitaji hayo.

"Wateja wote wa Tigo wanastahili kupokea tuzo; tunatarajia kukidhi mahitaji ya mteja ya kuwa na uzoefu usio na dosari kila wakati wanapowasiliana kwa chapa zetu.

Tunaamini kuwa wateja wetu watafurahishwa na zawadi hizi mpya ikiwa ni pamoja na bonasi kwa dakika, ujumbe mfupi wa maneno (SMS) au data wanazozawadiwa na hivyo kuimarisha utamaduni wao wa mawasiliano, "alibainisha Mpinga.

Na Dotto Mwaibale

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com