Mwanasheria MKuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki leo tarehe 24 Agosti 2017 amepata dhamana ya polisi na kuweza kuachiwa huru baada ya kushiliwa na jeshi hilo kwa siku mbili.
Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana ya Polisi kwa masharti ya kuripoti kituo cha polisi siku ya Jumatatu ya tarehe 28 Agosti 2017 wakati wowote akiwa na muda.
Tundu Lissu alikuwa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kusema makosa za Rais John Pombe Magufuli hadharani pamoja na kosa la uchochezi kufuatia matamka yako aliyoyatoa kuhusiana na kuzuiliwa kwa ndege mali ya Tanzania Bombadier Q400 nchini Canada kutokana na amri ya mahakama.
Mbunge Tundu Lissu amepata dhamana masaa machache baada ya Uongozi wa juu wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) kulitaka jeshi la polisi kumuachia Tundu Lissu na kumkamata Mbunge William Ngeleja ambaye alirudisha fedha za Escrow
"Hatuwezi tukaipata 87bn kwa kumuweka Tundu Lissu ndani au kwa kuwashutumu Wapinzani au watu kadhaa waliyoyaibua hayo, Unamuacha Willia Ngeleja amerudisha pesa za Escrow ni sawa amekiri kosa, mtu anayeeleza ukweli nchi inapata hasara anakamatwa, ni zaidi ya siku 4 tangu tamko la Chama litolewe hazijatoka hoja Serikalini zinazopinga kwa hoja na vielelezo kama tulivyolieleza" alisema Katambi
Social Plugin