Kutoka mjini Dodoma katika ukumbi wa St Gasper ulipofanyika mkutano mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF, mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Revocatus Kuuli ametangazwa matokeo ya uchaguzi Mkuu wa TFF kwa wajumbe, makamu na Rais wa TFF.
Aliyekuwa makamu wa Rais na kaimu wa Rais wa TFF Wallace Karia ametangazwa rasmi kuwa Rais mpya wa TFF kwa kupata jumla ya kura 95 na kuwashida Ally Mayay, Emmanuel Kimbe, Shija Richard, Iman Madega na Fredrick Mwakalebela.
Kwa ushindi huo sasa rasmi Wallace Karia atatawala nafasi ya Rais wa TFF hadi 2021 makamu wake akiwa ni Michael Richard Wambura aliyewashinda wagombea wenzake wengine watano.
Matokeo ya Urais
Kura ziliopigwa-128
Zilizoharibika-3
Iman Madega- 8
Mwakalebela- 3
Emmanuel Kimbe- 1
Shija Richard- 9
Ally Mayay- 9
Wallace Karia- 95 (Mshindi)
Social Plugin