Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye, ameahirisha mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa kwa ajili ya kumkabidhi rasmi kadi ya chama hicho aliyekuwa mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu.
Tukio hilo lilipangwa kuhitimisha tangazo la wema miezi kadhaa iliyopita kujiondoa Chama cha Mapinduzi(CCM) na akijiunga na Chadema.
Akizungumza na waandishi leo wakati akitangaza kuahirisha mkutano huo, Sumaye, ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu katika awamu ya Tatu, alisema tukio hilo limeahirishwa kwa sababu Wema ameshindwa kufika kutokana na kubanwa na ratiba za Mahakama.
"Hadi sasa Wema yuko ndani ya ukumbi wa mahakama akisubiri kesi yake inayomkabili, mawakili walitueleza kesi ingemalizika asubuhi na saa 6:00 mchana tungefanya moutano huu,” alifafanua Sumaye.
Wema anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya bangi ambayo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo.
Sumaye aliyekuwa amengozana na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee na Makongoro Mahanga, alisema Wema angekabidhiwa kadi na kuzungumza sababu za kujiunga Chadema.
Waandishi wa habari walifika ofisi za kanda hiyo kuanzia saa 5:00 asubuhi lakini ilipofika saa 6:00 mchana waandaji wa mkutano huo waliomba kusogeza mbele muda
Social Plugin