Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ZAIDI YA WAKAZI 3000 JIJINI TANGA KUNUFAIKA NA MIRADI YA MAJI YA TANGA UWASA


ZAIDI ya wakazi 3000 wanaoishi  katika eneo la Jaribu tena na Mwisho wa Shamba kata ya Maweni Jijini  Tanga wanatarajiwa kuepukana na adha ya uhaba wa maji safi na salama  iliyodumu kwa muda mrefu baada ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira Jijini Tanga kuwa pelekea mradi wa maji.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurungenzi Mtendaji wa Tanga UWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa alisema  kuwa mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.

Alisema  gharama za mradi huo hadi kukamilika kwake ni kiasi cha sh Mililioni 98, lakini kutoka na gharama  kuwa kubwa waliwashauri wananchi ili kuona namna watakavyoweza kufanya  kazi za kujitolea ili kukamilika kwa wakati.

Alisema kufuatia hali hiyo ndipo wananchi  walipoamua kushiriki katika kazi za kuchimba mitaro ambayo itaweza  kutumika kwa ajili ya kupitisha miundombinu ya mabomba kutoka Pongwe  hadi katika maeneo hayo yenye uhitaji.

“Tunawashukuru wananchi kwa ushirikiano waliounyesha wa kushiriki kwenye uchimbaji huo kwani wameweza kuokoa kiasi cha sh Mil 10 ambazo ingebidi  tuwalipe vibarua kwa ajili ya uchimbaji wa mitaro hiyo”,alisema Mgeyekwa.

Alisema mradi huo  umegawanyika katika awamu ambapo katika awamu ya kwanza unatarajiwa  kusambaza maji katika umbali wa Km 5.5 kutoka eneo la Pongwe hadi katika
mitaa ya Jaributena na Mwisho wa shamba.

Naye Mbunge wa Jimbo la Tanga Mussa Mbaruk alisema kuwa kukamilika kwa  mradi huo kwa haraka kutaweza kusaidia wananchi hao kuepukana na adha ya ukosefu wa maji iliyodumu kwa muda mrefu.

“Niwapongeze wananchi wa kata ya Maweni namna walivyoweza kujitolea kushirikina na serikali yao katika 
kumaliza changamoto zinazowakabili kwani hii inaonyesha kuwa ili  kuharakisha maendeleo ya sehemu husika kunahitaji ushirikishwaji wa  pande zote”alisema  Mbaruk.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata wa mtaa wa kichangani Ziada Ali alisema wakazi wa mtaa huo walilazimika kutembea umbali wa Km 5kwa ajili  ya kutafuta huduma hiyo kila siku.

Alisema mradi huo utakapokamilika itakuwa ni faraja kwa wananchi wa mitaa ya Jaribu tena  na Mwishi wa shamba pamoja na kuwapunguzu adha ya kwenda mwendo mrefu 
kwa ajili ya kutafuta huduma ya maji.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Maji Lucas Nyengo alisema kuwa kwa  takribani miaka minne wamekuwa wakiomba kupatiwa huduma hiyo lakini  wanashukuru kwa awamu hii kupatiwa mradi huo.

Alisema kufuatia shida ya maji ilidumu kwa muda mrefu 
waliamuakuunga mkono jitihada za mamlaka kwa kushiriki katika uchimbaji  wa mtaro ili kuharakisha mradi huo.

Alisema kutokana na shida ya maji iliyokuwa inawakabili
walilazimika kununua ndoo moja kwa kiasi cha sh 500 jambo ambalo ni gharama kubwa ukilinganisha na uhitaji wa huduma hiyo

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com