Kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir
***
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi-Unguja linawashikilia watu 20 kwa tuhuma za kukutwa wakifundishana kufanya mapenzi ya jinsia moja.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir amesema watu hao wamekamatwa wakati wakipatiwa mafunzo ya namna ya kuzitambua haki zao yaliyokuwa yakitolewa na taasisi iliyotambulika kwa jina la Bridge Initiative.
Hata hivyo hatua hiyo imekuja mwezi mmoja baada ya kauli ya mkuu wa mkoa huo ambaye pia ndiyo mwenyekiti wa ulinzi na usalama RC Ayoub Mahamoud kutamka kukomesha vitendo hivyo mara moja ambavyo vinaharibu sifa ya mkoa huo.
Mbali na hilo mkuu huyo wa mkoa akiliongoza Jeshi la Polisi tayari yuko katika operesheni ya kuzidhibiti biashara ya dawa za kulevya, ambapo zaidi ya Vijana 50 mkoani humo walikubali kuachana na matumizi ya dawa hizo.
Social Plugin