Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Tanga kuelekea Jijini Dar es salaam wamenusurika kufa baada ya basi walilokuwa wamepanda la kampuni ya Tashriff kuteketea kwa moto.
Kwa mujibu habari ambazo zimepatikana na kuthibitishwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba zimedai kwamba ajali hiyo imetokea saa nane machana katika eneo la Pongwe nje kidogo ya jiji la Tanga.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema wameona moshi ukitoka chini ya basi hilo ndipo wakapiga kelele na kusababisha dereva kusimama dakika chache baada ya hapo likaanza kuwaka moto.
"Tumesikia kelele kutoka kwa watu waliokuwa nje tukaona dereva kasimamisha basi muda si mrefu moshi ulianza kutoka mara moto ukalipuka"amesema Bahati Mussa abiria wa basi hilo.
Kamanda Wakulyamba amesema basi hilo ambalo lilikuwa likiendeshwa na Hemed Ali (35) lilikuwa na abiria 29 ambapo hakuna aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha.
"Hakuna aliyejeuhiwa wala kupoteza maisha imeteketea kwa moto"amesema Wakulyamba na kusisitiza kwamba jeshi la polisi linafanya uchunguzi kujua chanzo cha moto huo
Social Plugin