Habari zilizotufikia kutoka Tabora zinasema kuwa basi la kampuni ya Adventure lenye namba za usajili T992 BDT lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Mpanda mkoani Katavi limeanguka mbele ya kijiji cha Ipole wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Ajali hiyo imetokea leo jioni Jumamosi Septemba 2,2017.
Taarifa za awali zinasema Mtu mmoja amefariki dunia na zaidi ya 50 wamejeruhiwa.
Taarifa zaidi tutawaletea hapa kwenye blog yenu pendwa ya Malunde1 blog.Hizi hapa picha kutoka eneo la ajali
Taarifa zaidi tutawaletea hapa kwenye blog yenu pendwa ya Malunde1 blog.Hizi hapa picha kutoka eneo la ajali
Basi la Adventure likiwa limepinduka
Social Plugin