Mahakama imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo ikionyesha kuwa hana nia ya kuendelea na kesi dhidi yake.
Manji na watuhumiwa wenzake watatu walikuwa wakikabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na plate number mbili za magari ya serikali.
Watuhumiwa wengine walioachiwa huru kwenye kesi hiyo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja.
Social Plugin