Mwanamuziki Diamond Platnumz amemkubali mtoto aliyezaa na na Hamisa Mobeto na amesema jina alilotaka apewe mtoto huyo ni Dylan lakini kwa sababu za kutafuta umaarufu mwanamke huyo alimwita Abdul Nassib.
Amesema Hamisa alimwita mtoto huyo Abdul ambalo ni jina la baba yake mzazi ili iwe rahisi watu kufahamu kuwa mtoto huyo ni wa kwake baada ya kukubaliana kufanya uhusiano wao kuwa wa siri.
"Tulikubaliana na Hamisa Mobeto kuwa ujauzito huo usitangazwe kuwa ni wa kwangu, na alikubali lakini akawa anatangaza.
"Mpaka Mobeto anajifungua, nilikuwa nampa 70k kila wiki, nilimnunulia RAV4 na kabla hajajifungua nilimpa Tsh 7m ya kununua vitu.
"Sio kweli kwamba nilimkataa mtoto kama Hamisa anavyodai, bali alikuwa anatuma watu ili niseme sijamkataa watu wajue kuwa ni wangu.
"Zari anajua kuhusu mtoto wangu na Mobeto na hana tatizo, ila Mobeto anatengeneza mazingira nigombane na Zari kitu ambacho sitafanya.
"Wakati anajifungua nilimpa $3,500, nikamtafutia hospitali binafsi na baada ya kujifungua, nilimuomba mama yangu akamuone mjukuu
"Siku Hamisa Mobeto anajifungua sikuwepo Tanzania na niliporudi nilikwenda kumuona mwanangu na kulala naye hadi asubuhi.
“Mimi jina ninalolitambua ni Dylan hata niliposikia wamemwita Abdul nilisema poa tu lakini akija kwangu nitamwita ninalolitaka mimi kwa sababu nataka aitwe DD (D Square).” Amesema Diamond
Amesema alisikitishwa pia na kitendo cha mwanamke huyo kumualika baba yake katika sherehe ya kutimiza siku arobaini ya mtoto huyo akimdanganya kuwa angekuwepo.
“Walimwalika mzee Abdul na nguo wakampelekea ili ahudhurie, yote hiyo ili mradi tu wapate cha kuzungumziwa mitandaoni,” amesema.
Social Plugin