Kampuni ya udalali ya YONO imesimamia shughuli za kuuzwa kwa mnada gorofa lililopo Upanga mali ya kampuni ya Lugumi Enterprises Limited na kununuliwa na kampuni ya Al-Naeen Enterprises kwa shilingi Milioni 700.
Mnada huo wa maghorofa hayo na majengo mengine mawili ambayo yamekosa wateja kutokana na bei zake kuwa juu ukilinganisha na ukubwa wa jengo bado hayajapatiwa wateja.
Akizungumza wakati wa mnada huo, Mkurugenzi wa kampuni ya YONO Scolastica Kevela amesema kuwa Nyumba ambazo zimekosa wateja zinauzwa Shilingi Milioni 460 na zinapatikana eneo la Mbweni JKT Wilaya ya Kinondondi jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited inahusishwa na kashfa ya ubadhirifu wa fedha za serikali pamoja na kudaiwa kodi na TRA masuala ambayo yamepelekea kuuzwa kwa majengo hayo na kulipia kodi TRA.