HOSPITALI YA TEULE MUHEZA YAPATIWA MSAADA WA MASHUKA


Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Boniface Mhabe kushoto akipokea msaada wa mashuka 50 kutoka kwa Afisa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Sub Agro Trading anda Engineering,Neema Ng'unda kwa ajili ya wodi ya akina mama wajawazito kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza ilikiwa ni kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika kilimo wa pili kutoka kushoto ni  Afisa Mauzo wa Suba Agro Trading yenye makao makuu yake mjini Arusha,Shillaga Samweli 

*****
HOSPITALI ya Teule wilayani Muheza
Mkoani Tanga imepata msaada wa mashuka 50 kwa ajili ya kukabiliana na uhaba uliopo kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wagonjwa wanao kwenda kupata matibabu kutoka maeneo mbalimbali hasa vijijini.

Hatua ya uhaba huo unatokana na uchakavu wa wa mashuka unaotokana na kufubaa unaosababishwa na maji wanayotumia kufulia kutokana na uhaba wa maji hali iliyopelekea kuwepo
uhitaji kila wakati ili kuweza kukithi mahitaji ya wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu.

Hayo yalibainishwa jana na Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,  Boniphace Mhabe wakati akipokea msaada
wa mashuka 50 kutoka kampuni ya Suba Agro Trading na Engineering ambao ni mzalishaji wa mbegu bora zamahindi kwa kushirikiana na Cimmity taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mahindi na ngano.

Shuka hilo zilitolewa kwa ajili ya wodi ya wakina mama wajawazito  kwenye hosptali ya Teule Muheza,Hospitali ya wilaya ya Korogwe na wilaya ya Handeni lengo kubwa likiwa ni kuwaondolea changamoto zinazowakabili.

"Vitanda vipo vingi lakini tatizo kubwa ni mashuka na hili
linatokana  na asilimia kubwa kuchakaa kutokana na
maji lakini pia wakati mwengine yanabadilika rangi jambo ambalo limekuwa changamoto kwao.

Aidha alisema wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kusaidia  msaada huo ambao umefika wakati muafaka kwa kusadia baadhi ya vikwazo wanazokutana navyo wakati wa utoaji wa huduma za afya.

Awali akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,Afisa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo,Neema Ng'unda
alisema alisema wamekuwawakishiriki katika kuhamasisha kilimo Tanzania hususani kwa wakina mama ambao ndio nguzo kubwa hapa nchini kufikia mafanikio.

Alisema wamelenga wanawake kwa sababu ndio muhimili muhimu kwenye  jamii wa kuwawezesha wakina baba kwenye kulima kilimo bora ambapo kinaweza kuwainua kiuchumi.

"Lakini pia tunawashukuru wakulima wote Tanzania kwa kutumia mbegu zao kwa kulima kilimo cha kisasa ambacho
kinaweza kuwa mkombozi kijiinuakimaendeleo na kukuza mitaji yao",alisema.

Naye kwa upande wake,Afisa Mauzo wa Suba Agro Trading yenye makao makuu yake mjini Arusha,Shillaga Samweli
alisema zoezi hili limelenga kurudisha fadhila kwa wakina mama waTanzania maana ndiyo wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika
kilimo.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post