Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu kesi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji, October 6, 2017 baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wake wa mashahidi saba.
Hatua hiyo inatokana na Wakili wa Manji, Hajra Mungula kumueleza Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kwamba wamefunga ushahidi wao wa mashahidi saba ambapo baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkeha amesema kutokana na kufungwa ushahidi huo anatarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo, October 6, 2017.
Awali, Manji kupitia Wakili wake Mungula, aliiambia Mahakama hiyo kwamba angekuwa na mashahidi 15 lakini hadi leo September 26, 2017 ni mashahidi saba tu waliotoa ushahidi wao.
Katika kesi hiyo, Manji anadaiwa kati ya February 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.
Social Plugin