Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JENGO LA OFISI ZA MAWAKILI WA YUSUPH MANJI ZAVAMIWA NA WATU WASIOJULIKANA

Watu wanane wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wamevamia jengo la Prime House lililopo Mtaa wa Tambaza na kufanya uharibifu wa mali za wapangaji.

Jengo la Prime House lina ghorofa tano lipo jirani na ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Ilala jijini Dar es salaam.

Mwandishi ameshuhudia barabara ya kuingia eneo hilo ikifungwa kwa muda na polisi ambao walitumia magari yao kuziba njia na kuweka uzio wa utepe wa rangi ya njano.

Jengo la Prime House lina ofisi za kampuni mbalimbali, zikiwemo za mawakili wa Yusuf Manji ambazo zimevamiwa na wameondoka na nyaraka muhimu, duka la dawa na sehemu ya kufanya mazoezi gym.

Mmoja wa mawakili ambao wana ofisi katika jengo hilo, ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kwamba watu hao walipofika walimfunga mlinzi kwa kamba na kisha kuingia ndani kwa nguvu.

"Mlinzi ameniambia baada ya kuingia walipokuwa wakifanya upekuzi walikuwa wakisikika wakisema si huku tutazame ghorofa linalofuata si hili,” wakili huyo amemkariri mlinzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amethibitisha tukio hilo akisema limetokea kati ya saa nane na saa tisa usiku wa kuamkia leo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com