Wakazi wa Jiji la Mwanza wakiwemo waumini wa dini mbalimbali wameendelea kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkubwa wa injili ulioandaliwa na kanisa la kanisa EAGT Lumala Mpya chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kukola.
Jana mamia ya wananchi walijitokeza kwenye mkutano huo unaofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza na kukutana na mlipuko mkubwa wa injili kutoka
kwa watumishi wa Mungu akiwemo mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani chini ya huduma ya MORE International Ministry.
Aidha waimbaji Ambwene Mwasongwe, Mbilikimo Watatu, Samwel Lusekelo, Joseph Rwiza, Sam D, Havillah Gospel Singers na wengine wengi wameendelea kukonga nyoyo za
wahudhuriaji kwenye mkutano huo.
“Maandalizi ya mkutano huu ni ya kuvutia, tuna majukwaa matatu makubwa, vyombo vya muziki wa injili vizuri na pia tunatoa zawadi mbalimbali ikiwemo vyakula na nguo kwa
wanaohudhuria mkutano huu”,alisema Mchungaji Dkt.Kulola na kuwahimiza watu wote kufika kwenye mkutano huo ili wakutane na nguvu ya Mungu na kufunguliwa.
Mkutano huo ulianza juzi Jumatano Septemba 27 na utafikia tamati jumapili Oktoba Mosi, 2017 katika Uwanja wa Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza ambapo mamia ya wananchi waliokuwa wakiteswa na majini pamoja na magonjwa mbalimbali wanazidi kufunguliwa,
na leo huduma ya maombezi inaanza mapema majira ya saa nne asubuhi na mkutano utaanza saa tisa alasiri hadi saa 12 jioni.
Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani akihubiri kwenye mkutano huo-Picha na George Binagi-GB Pazzo
Watumishi mbalimbali wakiendelea kutoa huduma ya maombezi jana ambapo zaidi ya 20 walifunguliwa mapepo huku wengine wengi wakiponywa magonjwa mbalimbali
Mwimbaji wa muziki wa injili Ambwene Mwasongwe kutoka Dar es salaam akihudumu kwenye mkutano huo
Baada ya ibada, kanisa la EAGT Lumala Mpya kwa kushirikiana na wachungaji kutoka Marekani lilitoa zawadi kwa wananchi.
Tazama picha zaidi HAPA