Habari kutoka Kinondoni A mtaa wa Msisiri, karibu na CCM jijini Dar es salaam zinasema mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina la Emmanuel aliyekuwa anafanya kazi ya kupiga picha (photographer) amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na wivu wa kimapenzi.
Inaelezwa kuwa siku chache zilizopita marehemu alibaini kuwa mke wake alikuwa anatoka kimapenzi na mwanaume mwingine lakini alipomuuliza akakataa kusema ukweli ndipo ukaibuka ugomvi baina ya wawili hao.
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Msisiri Kinondoni A, wakishuhudia tukio hilo.
Social Plugin