Abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka (Udart) leo walikwama Kimara kutokana na kukosekana huduma kulikosababishwa na ajali iliyotokea Shekilango, Ubungo.
Vituo vya Udart vilivyoko Mbezi Mwisho hadi Ubungo vilifurika abiria baadhi wakiamua kutafuta usafiri mbadala.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Udart, Deus Bugaywa amesema gari moja liligonga lingine kwa nyuma hivyo kusababisha barabara kutopitika.
Bugaywa amesema baada ya mabasi ya Udart yaliyogongana kuondolewa, hivi sasa wanachofanya ni kuhakikisha abiria wote walio vituoni wanapata usafiri.
Social Plugin