Vijana wawili wanaosadikiwa kuwa wanajihususha na kuwateka waendesha bodaboda Mkoani Tabora wameuawa na wananchi wenye hasira baada ya mwendesha pikipiki kupiga kelele akiomba msaada alipokuwa amekabwa na wezi hao kwa lengo la kumpora pikipiki yake.
Kamanda wa Polisi Mkoani Tabora, Kamishina Msaidizi Mwandamizi Willibrod Mtafungwa amemtaja kijana aliyekuwa amekodiwa na vijana hao na kuwabeba kwa mtindo wa mshikaki, kwa jina la Haruna Bungala ambaye alikodiwa majira ya saa nne eneo la shule ya msingi Kitete ambapo walimpeleka kata ya Malolo na kuanza kumkaba.
Aidha kijana huyo Bungara ambaye alijeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali kwenye shavu la kushoto amesema kuwa kama si kupiga kelele alikuwa anauawa na waporaji hao lakini wananchi walijitokeza na kuanza kutoa adhabu hadi kifo na kuchomwa moto,
Kwa upande wa Mwenyekiti wa waendesha bodaboda amewapongeza wanachi kwa kutekeleza adhabu hiyo dhidi ya waporaji hao.
Social Plugin