Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) wakioneshwa na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Brigedia risasi zilizotolewa kwenye mwili wa Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba baada ya jana kushambuliwa wakati akiingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo-Picha na IKULU
****
Ikiwa ni siku tano tu zimepita tangu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Area D, Dodoma, tukio lingine kama hilo limetokea Dar es Salaam ambapo watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wamemshambulia kwa risasi Meja Jenerali Vincent Mritaba.
Tukio hilo limetokea jioni ya September 11, 2017 wakati Meja Jenerali Mritaba akiwa anaingia getini nyumbani kwake Tegeta ambapo alivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa risasi tumboni, begani na mguuni.
Hadi usiku wa jana Madaktari walikuwa wanaendelea na upasuaji kutoa risasi tatu tumboni na kushughulikia majeraha mengine.
Social Plugin