Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ODINGA : TUME YA UCHAGUZI KENYA IMEOZA..WALIOHUSIKA KUVURUGA UCHAGUZI WAWAJIBISHWE

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema tume ya uchaguzi nchini Kenya "imeoza".

Amesema maafisa wengi wakuu wa tume hiyo walikula njama kufanikisha wizi wa uchaguzi wa urais.

Bw Odinga amesema ni lazima viongozi waliohusika wawajibishwe na kusisitiza kwamba mitambo ya tume ya uchaguzi ni lazima iwekwe wazi kwa ukaguzi.

Kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga amesema uamuzi wa mahakama wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais yanaashiria mwanzo wa Kenya mpya.

Amesema majaji walionyesha kwamba mahakama zinaweza kuwa na uhuru na kusimama dhidi ya nguvu za marais Afrika.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com